Archives du GRILA
SASA! AFRICOM Kati ya Afrika - SASA! -- Tamko katika Sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Afrika Hamsini Ukombozi -- Azimio wa Kuadhimisha na Kusherekea Makumbusho ya Miaka Hamsini Tangu Kubuniwa Siku ya Ukombozi wa Afrika (Swahili)
SASA! AFRICOM Kati ya Afrika - SASA! -- Tamko katika Sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Afrika Hamsini Ukombozi -- Azimio wa Kuadhimisha na Kusherekea Makumbusho ya Miaka Hamsini Tangu Kubuniwa Siku ya Ukombozi wa Afrika (Swahili)
AFRICOM Nenda Nyumbani -

SASA! AFRICOM Kati ya Afrika - SASA!

Tamko katika Sherehe ya Maadhimisho ya Siku ya Afrika Hamsini Ukombozi


Azimio wa Kuadhimisha na Kusherekea Makumbusho ya Miaka Hamsini Tangu Kubuniwa Siku ya
Ukombozi wa Afrika

Mei 25, 2013
[NOTE: This current Swahili version is still under revision. Click here to read previous version of Document Previous version ]
"... Sisi kama viongozi wa dola na serikali za Afrika tukikusanyika jijini Addis Ababa;
Tukifahamu kwamba ni haki ya watu wote duniani kumiliki na kuamua nafsi yao;
Tukifahamu kwamba uhuru, usawa, haki na heshima ni lengo muhimu kufikia maazimio yetu kama watu wa Afrika;
Tukifahamu jukumu letu wa kuleta pamoja utajri wetu na mali yetu ili kuendeleza watu wote katika kutafuta ustawi kama binadamu; "

Tunauliza:
Je, nini hasa wosia ama urithi wa mkataba ilioandikwa na viongozi wazalendo hayati Modibo Keita na marehemu Sylvanos Olympio tarehe ishirini na tano mwezi wa tano mwaka wa elfu tisa sitini na tatu na kuadhinishwa na nchi huru za Afrika thelathini na tatu?

Pengine twaweza kusema kwamba hatimaye mkataba huu ambayo iilikaribisha Umoja wa Nchi Huru za Kiafrika haikufaulu kuunganisha WaAfrika. Takriban miaka hamsini baadaye, ingawaje Umoja wa Afrika imechukua pahala pa OAU, Afrika bado inajitahidi kutambua uwezo wake na kuhakikisha inajiamulia nafsi yake. Bado bara letu la Afrika imekwama katika matope ya unyonge inachoendelezwa na sekta ya kimataifa ya kufanya kazi iliotekwa nyara na mfumo wa ubeberu inaopinga vikali adili za umoja wa Afrika. Kusema kweli, taarifa ya hivi majuzi kutoka idara ya ulinzi huko Ufaransa yanena kwamba msukumo wa kuleta umoja baina ya Waafrika ni kinyume ya matakwa, maslahi na sera za Kimagharibi.

Leo tukiidhinisha miaka hamsini zilizopita popote tulipo, tuna ari, wajibu na lengo wa kuzika sera na kasumba ya ukoloni na ukoloni mambo leo katika kaburi la sahau. Kuanzia karne ya kumi na tisa na kuendelea hadi ya ishirini, ukoloni ulitapakaa kote barani Afrika. Mnamo mwaka wa 1885, ukoloni ilifanya hila na njama ya kihalifu na ubepari dhidi ya watu wa Kongo wakati Kongamano wa Berlin ilitangaza nchi ya Kongo kama "Eneo la Biashara Huru" kwanza duniani, kitendo ambacho kilizua enzi ya ubakuzi, unyakuzi na uvamizi wa kikoloni kilicho hatimaye gawanya na kusambaratisha bara letu la Afrika.

Hivi tukizungumza mwaka huu wa 2013 tunaona dhahiri kwamba kikosi cha kiimla kijulikanayo kama US Africa Command, maarufu AFRICOM, kutoka makao yao makuu jijini Stuttgart, Ujerumani, tayari yanapanga njama kueneza matawi yao kote barani Afrika wakitumia makinzano na vuta ni kuvute kadhaa za kisiasa, kiuchumi, kiitikadi na kijimbo zinazokumba na kuvuruga nchi nyingi za Afrika. Hata Ujerumani kwenyewe yenye historia ndefu za vita, wengi ya watu ambao wanasema Ujerumani ndipo nyumbani wanapinga vikali umwagikaji wa damu hivi wakisimama kidete na juhudi zetu na kupambana na umabavu wa kijeshi. Katiba ya Ujerumani katika kipengele ya 26 yapiga marufuku njama zote za vita au uvamizi kuendelezwa kutoka nchini mwao kwa sababu tukio kama hilo inaweza kuhatarisha hali ya amani na usalama miongoni ya watu. Na kipengele ya 25 yakariri kwamba sheria za kimataifa inataifisha iwe pia sheria ya Ujerumani na inapewa kipeo mbele juu ya sheria zote zingine.

Kwa hivyo, hali ya hizi njama za kihalifu zinakabidhi mahakama na sheria nchini Ujerumani haki ya kusikiza mashtaka zote kuhisiana na ukiukaji wa sheria za kimataifa bila kujali uraia wa watumuhiwa. Kama wanawake na wanaume sote tuna tumaini ya kutafuta amani, hali ya kujitawala na solidarity.

Kuambatana na sera zake za uvamizi na upanuzi dhidi ya Afrika, AFRICOM iliovumbuliwa na aliekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, inadai eti kwamba ina "linda usalama wa nchi ya Amerika kwa kuchangia nguvu za madola za Afrika kujihami dhidi ya vitisho za kimataifa". AFRICOM yadai kwamba kuchukua hatua hizo zitawezesha nchi za Afrika kuunda mazingira kusukuma gurudumo la maendeleo. Ni wazi dhahiri kwamba AFRICOM inajaribu kuanzisha kituo cha kijeshi barani Afrika ili ipate kugura kutoka Stuttgart ambako imekita makao makuu tangu mwaka wa 2008. Kikundi kiitwacho US Marine Forces Africa (MARFORAF) ilioratibisha mashambulio za kijeshi kote Afrika pia iko huko huko Stuttgart.
Hadi sasa, kulingana na karibu nchi zote za Kiafrika hazivutiwi kamwe na pendekezo la kuleta AFRICOM barani Afrika. Hata hivyo, nchi chache zimeshawishiwa na jaribio hili. Njama za AFRICOM zinahusu kupotoshwa akili kiitikadi na sera za kupiganisha nchi za Afrika popote wanaweza kufanya hivyo. Kwa kufuatilia sera zingine za NATO na kuiga maamuzi za kihaini za nchi kama Ufaransa, AFRICOM yaendeleza maslahi za nchi za Mabeberu na vibaraka vyao wa kicomprador kote Afrika. AFRICOM wakianzisha kituo cha kijeshi barani Afrika basi watapata nafasi ya kufyonza mali ghafi ya Afrika na kumilika sehemu muhimu kwao kisiasa uchumi. Isitoshe AFRICOM barani Afrika itokomesha ulafi wa mseto unaoubika ya BRIC (kumaanisha Brazil, Russia, India na China ) mbali na kuzuia mienendo za Waafrika kutafuta umoja barani Afrika.

Kusema kweli hakuna nchi yoyote mwanachama wa NATO inahitaji kuanzisha ama kumiliki kituo kikubwa cha kijeshi kama vile inavyokusudiwa na AFRICOM kwa sababu nchi hizi tayari yana vituo vyao na wanaweza kunufaishwa na mipango baina ya nchi zao na nchi binafsi za Afrika. Mbali na hapo sifa ya majeshi za takriban nchi zote za barani imezorota kwa sababu ya uhusiano wa karibu na wafanyi biashara wa kijeshi kutoka kwa nchi za kibeberu na kibepari ambao wana sifa mbaya ya kueneza njama za kigaidi zinazoenea popote ambapo kuna ukosefu wa maendeleo. Isitoshe, hawa hawa mabeberu wanafanya kazi usiku na mchana kuangamiza na kusitisha vugu vugu, miseto na miendendo zote za kuania demokrasia Afrika Kaskazini ama kuwasukumiza ama kuwahimiza vibaraka vyao Mashariki ya Kati kuzidi kuunga mkono serikali za unyama na udikteta.

Bara la Afrika imedhalilishwa kutokana sera potofu za mashirika kama Benki la Dunia (World Bank) na Mfuko la Fedha ya Kimataifa (IMF( kwa zaidi ya miaka thelathini, sera ambazo zimepunguza uwezo wa dola kushiriki katika shughuli za afya, elimu, miundo msingi na kinyume chake kuwasukuma wataalamu wawe madereva kuendesha sera za serikali katika nchi zetu za Afrika. Sera hizi zimesambaza dhana ndoto kuhusu demokrasia na kuondoa hisia za kisiasa kutoka kwa wananchi na kuwaambukiza nchi zetu karibu zote na virusi ya kutegemea wageni kutoka ngambo. Tukiangazia maswala za kijeshi, Afrika bado imegawanyika na kusambaratika mpaka hatuwezi kulinda ama kudhabiti jamii na nchi zetu kutokana na uvamizi wa kigeni kama vile tumeshuhudia Congo, Ivory Coast, Libya na Mali. Wakati huo huo hizi za kibeberu hawajakomesha kutisha amani, usalama na umoja wa nchi kama Sudan, Misri, Nigeria, Tunisia na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Nyakati kama hizi Umoja wa Mataifa inatumika kama chombo kutayarisha uvamizi wa majeshi ya NATO Afrika. Kifumba macho inayodhaniwa kana kwamba ni umoja wa zile nchi za Kiafrika zenye mwelekeo wa kijeshi katika shughuli za kulinda amani barani si kingine bali dhihirisho ya utawala wa kiimla wa Ubeberu. Kwa mfano, nchi thelathini na sita kutoka Afrika zilituma walio waliobandikwa kama kizazi kijao cha viongozi katika sekta ya ulinzi na usalama kwa warsha jijini Washington walihusishwa chini ya mwavuli wa kujenga utendaji kazi na kujenga nguvu ya kijeshi katika muktadha wa AFRICOM kiitwacho Theater Security Cooperations Programs (TSCP). Mradi wa The African Contingency Operations Training and Assistance (ACOTA) pia ni miongoni wa hizi mipango ya kuwafundisha wanajeshi kutoka Afrika na zimechangia pakubwa kuwafundisha majeshi kutoka mataifa kadha wa kadha katika shughuli za kulinda amani katika wadhifa wa Umoja wa Mataifa. Katika miaka kumi zilizopita, nchi nyingi za Kiafrika wameshiriki kwa mazoezi za kila mwaka dhidi ya ugaidi zifanyazwo Kaskazini and Magharibi ya Afrika ambao inajulikana kama FLINTLOCK. Mbali na hapo kuna AFRICA ENDEAVOUR ambacho kinajigamba kama nafasi ya kujenga ujuzi na maarifa katika Nyanja za mawasiliano ya ujasusi na upelelezi. CUTLESS EXPRESS nayo inaangazia mkururo wa sera za bahari na mabaharia kulinda usafiri za baharini katika maeneo za Afrika Mashariki na Bahari ya Hindi.

Kusema ukweli lazima kuwepo hali ya ukosefu wa usalama barani Afrika kuhalalisha hii hali ya kujipiga mabavu na kujigamba kwa majeshi. Twajua kwamba mitandao za magaidi na maharamia wa kisiasa ambao hawasikizi mtu ila wao ambao wanatisha utulivu ulimwenguni wakati ule ule wanaotisha hizo nchi za Kiafrika wanaoshambulia mara kwa mara. Hata hivyo hii ni chembe na kionjesho tu; ukweli wa mambo hususan imefichwa. Ukipiga darubini na kuchimba kutafuta kiini ya ugomvi na malumbano haya, utagundua kwamba chanzo ya mambo yana mizizi katika umasikini na ukosefu ya maendeleo.

Shida hizi ni matokeo za sera zilizo anguka mitihani kwa kupata suluhisho za kudumu kwa matatizo donda sugu kama kwa mfano uhalifu na usafiri haramu wa binadamu baina ya mipaka za nchi zetu kutokana na vita za mara kwa mara pamoja na vituko za kuchanganisha na kufadhaisa zinazohushiwa na zile makumpini za kibepari zinazoitwa " Juniors". Baadhi ya makampuni haya ni za kimataifa ambao wanafanya mipango za hila na magaidi na waasi ili wapore madini, utajiri wa kiasili na mali ghafi za Waafrika kabla ya kuziiba na kusafirisha nchini mwao kutafuta pesa na utajiri kwa nafsi yao wenyewe. Wakati fulani, tayari kuna njama zishambakwa mbeleni na wageni na mara tu kuna maeneo na majimbo ambazo " zimeokolewa" na waasi ambapo sasa kuna kisingizio wa kuzidisha usalama kwa ujumla hivyo kukaribisha na kuhalalisha majeshi kuingilia katika matukio za kisiasa, kiuchumi na kijamii. Nyingi katika serikali zinazo tawala nchi za Afrika wanahusika moja kwa moja katika hii ulanguzi na utapeli wa mali ya Afrika ama wakati wanahongwa na kunyamazishwa na vikwazo za kiuchumi ama kubembelezwa na asali ya kupora madini na mali ghafi zetu.

Kukaliwa kwa majeshi zetu za Afrika na mabeberu kutoka Amerika Kaskazini na Bara Ulaya pamoja na hofu ya kushudia AFRICOM ikikita kambi barani Afrika- tukitumia mfano wa hivi majuzi tulipoona majeshi ya Ufaransa yakivamia Mali ni pingamizi na kizuizi katika jitihada zetu ya kutafuta muungano wa kiuchumi, kisiasa na kijamii barani Afrika. Jambo la kuhuzunisha ni kwamba Afrika yaendelea kutafuta kivuli chini ya mwavuli wa NATO. Kusema ukweli AFRICOM na NATO wameingiliana na kuunganishwa kiasa cha kwamba hatuwezi kujua wapi AFRICOM yaishia na NATO kuanzia. Kwa mfano, mwanzoni wa Mei mwaka huu wa 2013, Katibu Mkuu wa NATO Jemedari Rasmussen alipokea tuzo kuu kutoka kwa Atlantic Council huko Washington. NATO na AFRICOM pamoja ni wahusika na watuhimiwa wakuu katika sera za kusambaratisha na kugawanya Afrika.

Baadhi ya vipengele muhimu katika historia ya Afrika katika hizi miaka hamsini tunaokumbuka na kuadhimisha leo tarehe ishirini na tano, mwezi wa tano zinahusu mipango ya wabeberu kukwamisha hisia za kutafuta uhuru na kujitawala; mapinduzi za kijeshi dhidi serikali za kimapinduzi na kupenda maendeleo; vikwazo dhidi hatua ya kungoa utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini; sera za kigeni za kuyumba yumba ya Serikali ya Amerika ndani ya Somalia na Sudan; mazungumzo na mtandao wa kigaidi ya Al Qaeda; mashambulizi na wanamgambo wenye hisia za siasa kali za Kiislamu kabla mashambulizo New York mnamo mwezi wa tisa tarehe kumi na moja mwaka wa elfu mbili na moja na sera za kupinga ugaidi zilizoibua; mnamo mwaka wa elfu mbili na mbili kulivumbuliwa mpango wa kupambana na ugaidi katika nchi tatu za jimbo la Sahel. Miaka mitatu baadaye mpango huo wa Trans Sahara Counter Terrorist Initiative (TSCTI) ulipanuliwa kushirikisha mataifa mengine tano.

Baadaye mpango wa East Africa Counter-Terrorist Initiative (EACTI) kilianzishwa Afrika Mashariki ikileta pamoja nchi sita. Mwaka huo huo wa elfu mbili na tano NATO ilikubali mwaliko wa Umoja wa Africa kuingilia maswala za Darfur. Miaka miwili baadaye, NATO ilianzisha utafiti iliozaa mabrigadi ziijulikanayo kama African Standby Force (ASF) ambao lengo lake yaadiwa ni imarisha amani barani Afrika. ASF itaanza kazi yake mwaka wa 2015.

Tukizungumzia Afrika kwa ujumla matukio haya yote yamaanisha ukiukaji wa haki yetu kama Waafrika kujiamulia nafsi yetu. Wakiwa tayari kushambulia nchi zetu, NATO na AFRICOM hawatawajibu kutafuta ushauri ama mwelekeo kwa mtu yo yote ila ofisa wao wa kusimimamia ushirikiano kati ya majeshi maarufu kwa kimombo kama Senior Military Liaison Officer (SMLO) ambae ndio mwakilishi wa NATO na AFRICOM na Umoja wa Afrika (AU).

Sisi wakereketwa tunaopambania uhuru, umoja na ustawi ya Waafrika popote walipo tunajukumu kujizatiti na kuhamasisha watu wote wawe ni mwamko sio tu wa uzalendo lakini kile kifipako kilele cha mtazamo wa ukimataifa; mwamko itakao wafufue and kuamusha wale miongoni mwetu walio katika tabaka ya mapebari mchwara pamoja na walala hoi na wachochole wote watambue mapema kwamba ongezeko ya majeshi na umajeshi haitupeleki popote. Kuongezeka kwa mfumo wa umajeshi itazidisha makinzano, migogoro barani Afrika.

Tukitaka Afrika ijikomboe, lazima tungoe vituo vyote vya majeshi za kigeni barani Afrika.

Tuwe na imani na tuzingatie juhudi na mradi ya kujenga Jeshi Moja la Kusimamia Afrika nzima. Jeshi ambalo lengo lake kuu na pekee ni kulinda bara letu na kuchangia pakubwa kuboresha amani chini ya mwito tukufu la Amani Afrika!

Mwito wetu wa Ukombozi wa Afrika yamaanisha kwamba lazima tujitegemee kuleta umoja wa Afrika na ya Waafrika;

Makusudio yetu za kiitikado zinapinga vikali mwenendo wa ukoloni mamboleo tunaoshuhudia sasa wa viongozi wengine kujifanya vibaraka na vibarakala wa nchi za kigeni na za kibeberu. Majeshi zetu hazifai kuwa watumwa na mahabusu ya wageni ambao ndio wanzilishi na wafadhili wa vita nyingi hapa Afrika.

Tukilinda maslahi zetu kama Waafrika tutegemee umoja wetu kama Waafrika; tusiwasubiri ama kutegemee NATO ama AFRICOM watusulushie shida zetu.

Pamoja, tuunge mkono shughuli za kuelimisha na kuhamasisha kisiasa vijana wetu kote Afrika.

AFRICOM: Ondoka Afrika!

AFRICOM: Ondoka Afrika!
Afrika ni ya Waafrika, wawe barani Afrika ama popote walipo duniani!

Tumekataa kata kata vituo vyote vya majeshi za kigeni Afrika!

Amerika, Ondoka Afrika Mara Moja!

Tumekataa ugaidi wa kijeshi na vituo vya kijeshi barani Afrika

Ondoka Mara Moja!

Ondoka Mara Moja Kutoka Chagos!

Ondoka Mara Moja Kutoka Diegi Garcia!

Ondoka Mara Moja Kutoka Libreville!

Ondoka Mara Moja Kutoka Sao Tome!

Ondoka Mara Moja Kutoka Ceuta!

Ondoka Mara Moja Kutoka Ndajemena!

Ondoka Mara Moja Kutoka Djibouti!

Ondoka Mara Moja Kutoka Trpoli!

Tumekataa kata kata makumpuni za kibeberu na kinyangiro ya kutapeli na kupora madini, mali ghafi na mashamba zetu!

Tumewakemea viongozi vibaraka na vibarakala- wakoloni mamboleo wanao ramba matako ya wabeberu!

Tupiganie demokrasia, haki, mapinduzi na ukombozi wa Afrika!

Afrika ni Moja!

Dada na Ndugu sote tupiganie Afrika
Group for Research and Initiative for the Liberation of Africa

Sisi tulidhinisha Azimio Go Home AFRICOM;
GRILA - Group for Research and Initiative for the Liberation of Africa
We endorse the Declaration Go Home AFRICOM;
1. Forum du Tiers Monde (Samir Amin ; Bernard Founou)
2. Fondation Frantz Fanon (Mireille Fanon- Mendes-France)
3. HANKILI SO AFRICA (Koulsy Lamko) ;
4. AfricAvenir International
5. Black Agenda Report (Glen Ford) ;
6. Arbeitskreis Panafrikanismus München (Dipama Hamado)
7. Revival of Panafricanism Forum (RPF) (Gnaka Lagoke) ;
8. INSTITUT TUNISIEN DES RELATIONS INTERNATIONALES (ITRI) (Ahmad Manai) ;
9. Yash Tandon, Former Executive Director of the South Center ;
10. Diasporic Music on Uhuru Radio ;
11. Network for Pan Afrikan Solidarity - Ajamu Nangwaya, University of Toronto ;
12. Emira Woods - IPS ;
13. Forum Africain des Alternatives
14. (ARCADE) Africaine de Recherche et de Coopération pour l'Appui au Développement Endogène , (Demba Dembélé)
15. Afrika Kulturprojekte e.V.
16. Dr Horace Campbell - Syracuse University
17. Dr Saër Maty Bâ - Somerset, United Kingdom;
18. Dr Sanou Mbaye,
19. Dr. Boniface Mabanza (Kirchliche Arbeitsstelle Südliches Afrika KASA)
20. Dr Amzat Boukari-Yabara (Ligue Panafricaine - Umoja)
21. Dr Werner Ruf (AG Friedensforschung)
22. Berlin Postkolonial e.V. (Mnyaka Sururu Mboro und Christian Kopp)
23. Ginga Eichler, Dipl.-Afrikanistin
24. Dr. Lutz Holzinger, (Journalist and Writer in Vienna)
25. Ababacar Fall, Dakar Senegal
26. Dr Henning Melber, The Dag Hammarskjöld Foundation, Uppsala/Sweden
27. Wolf-Dieter Narr, Komitee für Grundrechte und Demokratie
28. Joanès Louis (Université Populaire Kwame Nkrumah)
29. Werner Kersting, Vorsitzender Stoffwechsel e.V.
30. Carina Ray Assistant Professor, History Department, Fordham University,Bronx, New York
31. Hans-Peter Laubentha
32. Dr. Bärbel Schindler-Saefkow, Deutscher Friedensrat e.V
33. Elikia M'Bokolo, Directeur d'Etudes, EHESS
34. Siegfried Wittig, Berlin
35. Afrika Netzwerk Bremen
36. Wikopuli, Andreas Schlüter
37. Andrea Williams MA, MBA Director, Programmes/Administration Grove Broadcasting Co. IRIE FM Jamaica
38. Marita Blessing, MenschenEchte!-KreAktiv
39. Niema Movasat, Member of German Parliament, DIE LINKE
40. Marika Bruhns
41. Wade Mbaye Thioune, Urbaniste
42. Glokal e.V., Daniel Bendix
43. Alice Cherki, Psychiatre, Psychanalyste44.
45. Dr. Werner Ruf , Chattenweg 32
46. Evelyn Dürmayer, Kleeblattgasse
47. Dr. Helmut Küster, Germany
48. Dr. habil. Jürgen Kunze, Afrikanist/Soziologe, Leipzig
49. Elena Ball
50. Alisa Neuberger unterstützt Euch, Liebe Grüße aus Salzburg